Wauaji wa Kusini Wauawa

LINDI: Yanga imerejea kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania bara baada ya kuitandika Namungo FC 3-1 katika mchezo uliomalizika mda mchache uliopita Uwanja wa Majaliwa Ruangwa Lindi.

Mabao ya Yanga kwenye mchezo huo yamewekwa nyavuni na Mudathir Yahya dakika ya 54, Clement mzize ’57’ na Stephane Aziz Ki 62, Ibrahim Bacca amejifunga na kuipa Namungo goli la kufuta machozi ’69’.

Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha alama 46 na kuchupa hadi nafasi ya kwanza na kuishusha Azam Fc nafasi ya pili kwa alama 44 huku Simba wakiwa nafasi ya tatu na alama 36.

Namungo FC wamesalia nafasi ya saba wakiwa na alama zao 23 baada ya kushuka dimbani mara 20 msimu huu.

Habari Zifananazo

Back to top button