Wawekezaji sekta ya mawasiliano wakaribishwa Tz

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Khamis Abdulla amesema wizara hiyo ipo tayari kushirikiana na wawekezaji walioonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya mawasiliano nchini.

Kiongozi huyo amesema hayo leo Septemba6, akiwa jijini Beijing, nchini China mara baada ya kushiriki mazungumzo kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na wawekezaji na viongozi wa kampuni mbalimbali zilizopo China ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi nchini humo.

Abdulla amesema wizara iko tayari kushirikiana na wawekezaji hao na imeandaa programu itakayojulikana kwa jina la “From the Peak of Mount Kilimanjaro to Space” itakayohusu uundaji na urushaji wa satelaiti itakayoanza mwaka huu.

SOMA:  China wekezeni Tanzania – Prof Mkumbo

Wawekezaji walioonesha nia ya kuwekeza upande wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ni kampuni tatu ambazo ni China Academy of Space Corporation (CASC) inayojishughulisha na masuala ya uundaji na urushaji wa satelaiti.

Kampuni nyingine ni China Electronics Corporation iliyoonesha nia ya kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza vifaa vya TEHAMA pamoja na Kampuni ya Transsion Group.

SOMA: Rais Samia kuanza ziara China

Katika mkutano huo, Rais Samia amekuwa na mazungumzo na viongozi wa Kampuni za China Academy of Space Corporation (CASC), China Electronics Corporation, Transsion Group, Weihua Group, China Railway Construction Corporation (CRCC) pamoja na Acme Consultant Engineers PTE Limited na CND zote za China.

Habari Zifananazo

Back to top button