Waziri Mkuu akutana na Mwenyekiti AUPF

WAZIRI Mkuu, Kasim Majaliwa amekutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wa Japan cha Urafiki na Afrika (Africa Union Parliamentarians Friendship)-AUPF-, Ichiro Aisawa, kwenye Ofisi za Bunge la Japan.

Katika mazungumzo yao wamejadili kuhusu kuendeleza urafiki kati ya Bunge la Tanzania na Bunge la Japan.

Pia, wamejadili kuhusu masuala mbalimbali ya uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Japan, pamoja na kumkaribisha mwenyekiti huyo kutembelea Tanzania ili kujionea vivutio mbalimbali ya utalii.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button