Waziri Mkuu ashiriki Great Ruaha Marathon

IRINGA; Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 06, 2024 ameshiriki katika mbio za Great Ruaha Marathon 2024 zilizofanyika katika hifadhi ya Ruaha, mkoani Iringa.

Isome pia:https://habarileo.co.tz/majaliwa-atoa-maelekezo-vikundi-vya-jogging/

Mbio hizo zinalenga kukuza utalii wa Kusini na kutoa hamasa kwa jamii kuhifadhi mazingira kwenye vyanzo vya maji vya Mto Ruaha mkubwa.

Advertisement

Isome pia:https://habarileo.co.tz/mambo-yaiva-great-ruaha-marathon/

Aidha, lengo jingine ni kuhamasisha mazoezi na afya bora.