Waziri Mkuu mpya mtarajiwa Japan huyu hapa
CHAMA kinachotawala Japan, Liberal Democratic Party (LDP), kimemchagua Shigeru Ishiba kuwa kiongozi wake mpya huku mwanasiasa huyo mkongwe akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo.
Wagombea tisa wamewania nafasi ya uongozi wa LDP, ambayo imeongoza Japan kwa muda mrefu, baada ya mwezi uliopita Waziri Mkuu Fumio Kishida kutangaza kuwa hatagombea tena.
SOMA: Japan kutoa tril 70/- za miradi, mazingira Afrika
Yeyote anayechaguliwa kuwa mkuu wa LDP hutangazwa kuwa Waziri Mkuu chama hicho kinapokuwa na wingi wa kura bungeni.
Ishiba mwenye umri wa miaka 67 aliongoza katika kura nyingi za maoni, hiyo ikiwa mara yake ya tano na amesema ni nafasi yake ya mwisho kugombea uongozi LDP.
Mshindi wa uongozi wa LDP huamuliwa na kura za ndani ya chama kuliko za umma.
Mbio za kuwania uongozi huo zilianza na wagombea tisa kabla ya kubakia kati ya Ishiba na Sanae Takaichi, ambaye aliwania kuwa kiongozi wa kwanza mwanamke wa Japan.