Waziri Simbachawene ahimiza weledi miradi ya umma

DAR ES SALAAM; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amezihimiza taasisi za Serikali, ikiwemo Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuendelea na kutekeleza miradi ya umma kwa weledi na ufanisi

Simbachawene ameyasema wakati kukagua banda la TBA kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Alisema ni vema taasisi za umma ikiwamo TBA kutekeleza miradi ya umma kwa welezi na ufanisi ili kufanikisha malengo ya Serikali katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Aidha Simbachawene alitumia fursa hiyo kupongeza kazi bora ya ujenzi inayotekelezwa na Wakala na kuonyesha kuridhishwa na ubunifu na ubora wa majengo yanayojengwa na wakala huo.

“TBA mnafanya kazi nzuri katika ujenzi wa majengo ya Serikali. Hata jengo la Wizara ya Utumishi mmejenga ninyi, ni jengo zuri na linavutia. Hongereni sana.”

Katika banda la TBA, wananchi wanapata fursa ya kujifunza kuhusu miradi ya ujenzi inayotekelezwa na wakala huo, pamoja na kuona mchango wake wa maendeleo kwenye Sekta ya ujenzi

TBA ni miongoni mwa taasisi za umma zinazoshiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka huu ambayo yatafikia tamati yake Juni 23 mwaka huu yamebeba kaulimbiu isemayo “Himiza matumizi ya mifumo ya kidijiti ili kuongeza upatikanaji wa taarifa na kuchagiza uwajibikaji.”

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button