WAIGIZAJI Wema Sepetu, Irene Uwoya, Zuwena Mohamed, (Shilole) na Kajala Masanja wamejitolea taulo 30,000 zenye thamani ya Sh milioni 6.
Wema aliwapigia simu wenzake na kutoa ahadi kila mmoja alisema anachoweza kuchangia kwenye taulo hizo.
“Nawashukuru Irene Uwoya amesema atatoa taulo elfu 10000, sawa na Sh milioni 2, Shilole taulo 5000 swa na Sh milioni 1 na Kajala amesema atachangia taulo 15000 sawa na Sh milioni 3.” amesema Wema
Pia amewaomba watanzania wote kumpa ushilikiano katika kampeni yake ya kumsaidia mtoto wa kike asome kwa raha.