Wizara, PURA kuimarisha utoaji habari miradi ya mafuta, gesi

DAR ES SALAAM: Wizara ya Nishati na Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) zimekutana kujadili mikakati ya kuimarisha utoaji wa elimu kwa umma kuhusu miradi ya utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia inayotekelezwa nchini.

Majadiliano hayo yaliyofanyika Oktoba 13, 2026 katika Ofisi za PURA Jijini Dar es Salaam yalihudhuriwa na wajumbe mbalimbali akiwemo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Nishati, Nteghenjwa Hosseah na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wazawa na Uhusishwaji wa Wadau kutoka PURA, Charles Nyangi.

Akizungunza katika kikao hicho, Nteghenjwa amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia lakini bado elimu kwa umma kuhusu miradi hii ni haijatolewa ipasavyi, hali inayofanya wananchi kutokuwa na uelewa mpana wa miradi inayotekelezwa.

“Kwa sasa tuna miradi inayoendelea kutekelezwa mkondo wa juu wa petroli ukiwemo mradi wa uchukuaji wa data za mitetemo za 3D katika Kitalu cha Lindi – Mtwara, mradi uchukuaji wa data za mitetemo za 2D katika Kitalu cha Eyasi – Wembere na maandalizi ya uchimbaji wa visima vya gesi asilia katika Kitalu cha Ruvuma. Hata hivyo, uelewa umma wa Watanzania kuhusu miradi hii na faida zake bado ni mdogo” alieleza Nteghenjwa.

Alisema pia pamoja na kwamba miradi hiyo inahusisha masuala ya kitaalamu, Wizara ya Nishati na Taasisi zake zinajukumu la kuhakikisha kuwa umma wa watanzania wanapata taarifa za utekelezaji wa miradi kwa lugha nyepesi na kwa wakati ili kusaidia kuongeza uelewa wao katika miradi hiyo.

Kwa upande wake, Nyangi amesema kuwa PURA itaendelea kuongeza nguvu katika utoaji wa habari kwa umma kuhusu miradi inayotekelezwa sambamba na kuwajengea uwezo wanahabari kuhusu masuala ya mkondo wa juu wa petroli.

“Pamoja na kutumia vyombo mbalimbali vya habari katika utoaji wa taarifa, PURA imeendelea kuwezesha mafunzo kwa wanahabari na kutoa fursa kwa wanahabari kutembelea maeneo ambayo miradi ya mkondo wa juu wa petroli inatekelezwa nchini kwa lengo la kuongeza uelewa wa wadau hawa muhimu katika kuhabarisha umma” aliongeza Nyangi.

Habari Zifananazo

10 Comments

  1. Right here is the right blog for everyone who wishes to understand this topic.
    You realize a whole lot its almost tough to argue with
    you (not that I really will need to…HaHa). You
    certainly put a fresh spin on a topic that has been discussed for a long time.

    Wonderful stuff, just wonderful!

  2. موقع Code Siya9а هي منصة تعليمية مجانية
    يساعد الراغبين في الحصول على رخصة السياقة على تعلم كود
    السياقة المغربي بطريقة
    مبسطة ومناسبة للمبتدئين.
    تصفح شروحات قانون السير المغربي التي تشمل علامات الخطر والمنع والإجبار والإرشاد مع تفسيرات واضحة تساعدك على تحسين معرفتك بقواعد الطريق.

    يوفر Codee Siya9a مجموعة من تمارين المراجعة ومقالات توضيحية لمساعدتك على مراجعة
    دروس السياقة. سواء كنت تبحث عن دروس Permis Ԁе
    conduire Maroc، يمكنك مراجعة قواعد الأسبقية من خلال محتوى مناسب للتعلم الذاتي.
    تساعدك منصة Code Siya9a على تطوير معرفتك بالتشوير الطرقي مع إمكانية
    التدرب على الأسئلة أكثر من مرة.
    استعد لامتحانالسياقة بثقة مع Code Siya9а واستفد من دروس واضحة ومفيدة تساعدك على التحضير
    لرخصة السياقة قبل التقدم لاختبار السياقة.

  3. PURA’s initiative to break down complex 3D seismic surveys in Lindi-Mtwara reminds me of my college days in petroleum engineering, when I kept bookmarking the to see if my semester scores were strong enough for exploration field training. Demystifying these technical projects will definitely help motivate students aiming to join the energy sector.

  4. Kuhusu mradi wa uchukuaji wa data za mitetemo ya 2D katika Kitalu cha Eyasi–Wembere, nilijaribu kutafuta taarifa za kina zaidi za kiufundi mtandaoni ili kuelewa maendeleo yake, lakini badala yake nikaishia kufungua ukurasa wa アークナイツ公開求人ツール info nilipokuwa nikijaribu zana tofauti za utafutaji wa data. Ni muhimu sana kwa PURA kutoa elimu kwa lugha nyepesi kama walivyojadili, maana uelewa wetu wananchi kuhusu miradi hii mikubwa ya nishati bado unahitaji kuimarishwa.

  5. Uchukuaji wa data za mitetemo za 3D katika Kitalu cha Lindi – Mtwara unaonyesha ukubwa wa kazi inayofanyika, na kama unavyoona kwenye mfano wa Hero Siege Database overview kuhusu mpangilio wa takwimu, uwazi wa taarifa utasaidia sana kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu rasilimali zao.

  6. Uchukuaji wa data za mitetemo katika Kitalu cha Eyasi–Wembere na Lindi–Mtwara unaweza kuwa hatua muhimu, lakini kurahisisha tu taarifa hakutajenga uelewa thabiti bila mfumo wa uwazi kama unavyoonekana kwenye 貓咪大戰爭資料庫 homepage inayowapa watumiaji uwezo wa kuchambua takwimu za msingi wao wenyewe.

  7. Nteghenjwa Hosseah rightly points out that translating complex 3D seismic surveys from Lindi–Mtwara into accessible language is essential, yet the bigger implicit hurdle is helping communities forecast tangible economic yields from these reserves. Much like evaluating agricultural investments where you might consult Stardew Valley Crop Calculator tips to weigh input costs against expected returns, citizens need clear economic models to understand how upstream exploration translates into local prosperity. Until PURA provides transparent projections of civic benefits, technical simplifications alone won’t fully bridge the public engagement gap.

  8. Kuhusu data za mitetemo za Kitalu cha Lindi–Mtwara zilizotajwa na Nteghenjwa, mtu anayeanza kupakua ripoti hizo mtandaoni anapaswa kuangalia kwanza usalama wa faili husika, hivyo kutumia SHA256 Online site ili kuthibitisha checksum ya nyaraka hizo ni hatua muhimu ya kiusalama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button