Wizara ya Afya yaja na vipaumbele 10

WIZARA ya Afya imeainisha Vipaumbele kumi (10) vitakavyotekelezwa kwa mwaka 2025/26 , Bunge limeelezwa.

Akiwasilisha bungeni hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2025/2026, Waziri wa Afya Jenista Mhagama, amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni:

“Kuimarisha huduma za kinga dhidi ya magonjwa ya kuambukiza yakiwemo magonjwa milipuko, magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, magonjwa yasiyoambukiza na huduma za Lishe.

“Kuimarisha upatikanaji na ubora wa huduma za afya zinazotolewa katika ngazi zote kuanzia Zahanati hadi Taifa; Kuimarisha mifumo ya ugharamiaji wa huduma za afya nchini ikiwa ni pamoja na kuendelea na utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote.

“Kuendelea kufanya tafiti na kuhimiza matumizi ya matokeo ya tafiti hizo kwa maeneo ya kimkakati; Kuimarisha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga.

“Kuimarisha upatikanaji na uendelezaji wa wataalam katika Sekta ya Afya kwa fani za kati, ubingwa na ubingwa bobezi;

“Kuimarisha huduma za matibabu ya ubingwa na ubingwa bobezi pamoja na kuimarisha tiba utalii nchini; Kuendeleza na kusimamia afua za Tiba Asili na Tiba Mbadala.

“ Kuimarisha upatikanaji wa huduma za tiba dhidi ya magonjwa ya kuambukiza, magonjwa yasiyoambukiza na magonjwa ya mlipuko na Kuimarisha huduma za afya ya akili, huduma za utengamao hususan kwa watoto, wazee na watu wenye ulemavu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button