Yanga bingwa 2024/25

DAR ES SALAAM; YANGA imetetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2024/25, baada ya leo kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mtani wake Simba Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Kutokana na matokeo ya mchezo huo wa kiporo uliokuwa awali uchzwe Machi 8, 2025, Yanga imefikisha pointi 82 ikiwa kileleni mwa msimamo, ikiiacha Simba ikishika nafasi ya pili kwa pointi zake 78.
Mabao ya Yanga katika mchezo huo yalifungwa na Pacome Zouzoua dakika 66 kwa penalti na Clement Mzize dakika ya 86.