MAURITANIA;HESABU Yanga zimekubali. Pengine ndivyo unavyoweza kuzungumzia matokeo ya mchezo uliomalizika muda mfupi uliopita kati ya Al Hillal na Yanga uliochezwa nchini Mauritania na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 0-1.
Yanga ilikuwa inahitaji ushindi leo ili kufikisha pointi 7, iwe na kazi moja tu ya kushinda mchezo wa mwisho dhidi ya MC Alger Jumamosi ijayo Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na kufuzu hatua ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga inaendelea kushika nafasi ya tatu nyuma ya MC Al ger inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 8 na vinara Al Hillal wenye pointi 10 ambao tayari wamefuzu robo fainali.
Bao hilo pekee katika mchezo huo wa Kundi A lilifungwa kipindi cha kwanza na Aziz Ki.