Yanga kuanza kutetea ubingwa Ligi Kuu leo

BINGWA wa Kombe la Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga leo inaanza kampeni ya kutetea taji hilo ugenini dhidi ya Kagera Sugar.

Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

SOMA: Yanga vs Simba Ngao ya Jamii Agosti 8

Katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu timu hizo kukutana Mei 8 mwaka huu kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam Yanga ilishinda kwa bao 1-0.

Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo KMC itakuwa wenyeji Coastal Union kwenye uwanja wa KMC Complex, Kinondoni Dar es Salaam.

KMC na Coastal Union zilitoka suluhu katika mchezo wa mwisho wa Ligi kati ya timu hizo Mei 28 mwaka huu.

Yanga, Coastal Union na Azam ambayo imecheza Agosti 28 dhidi ya JKT Tanzania zimechelewa kuanza ligi kutokana na majukumu ya kimataifa.

Habari Zifananazo

Back to top button