NI ushindi pekee utakaoihakikishia Yanga kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika(CAFCL) katika mchezo wa mwisho wa michuano hiyo hatua ya makundi dhidi ya MC Alger kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam leo.
Yanga ipo nafasi ya tatu kundi A ikikusanya pointi saba baada ya michezo mitano nyumba ya MC Alger yenye pointi nane.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Desemba 7 huko Algeria, Yanga ilipoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya MC Alger.
Al Hilal itakayomaliza michezo ya makundi ugenini dhidi ya TP Mazembe inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi 10 wakati Mazembe inashika nafasi ya nne mwisho wa msimamo ikiwa na pointi mbili.
Michezo mingine ya Ligi ya Mabingwa Afrika inayopigwa leo ni kama ifuatavyo:
KUNDI C
Al Ahly vs Orlando Pirates
CR Belouizdad vs Stade D’abidjan
KUNDI D
Esperance vs Sagrada Esperanca
Pyramids vs Djoliba AC