Yanga kurejesha makali Ligi Kuu leo?

Wachezaji wa kikosi cha Yanga wakifanya mazoezi

BAADA ya rekodi ya kutopoteza mchezo wala kufungwa bao raund nane kuingia doa, klabu ya Yanga leo inashuka dimbani dhidi ya Tabora United katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.

Yanga ilipoteza mchezo iliopita wa Ligi Kuu dhidi ya Azam kwa bao 1-0.

Advertisement

SOMA: Yanga kuanza kutetea ubingwa Ligi Kuu leo

Yanga ipo nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 24 baada ya michezo tisa wakati Tabora United inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi 14 baada ya michezo 10.

Mara ya mwisho timu hizo kukutana Ligi Kuu Mei 25, Yanga iliibuka mshindi kwa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United.