Klabu ya Yanga imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo, Shekhan Ibrahim Khamis kutoka JKU ya Zanzibar kwa Mkataba wa miaka mitatu.
Yanga imethibitisha kumnasa mchezaji huyo kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii hii leo.
Shekhan alikuwa sehemu ya kikosi cha Zanzibar kilichoshiriki CECAFA U18 mwaka huu 2023 Kenya.