KLABU ya Yanga imepangwa kucheza na Vital’O FC ya Burundi katika hatua ya kwanza ‘Preliminary’ ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF) msimu wa 2024/2025.
Droo iliyochezeshwa muda huu na Shirikisho la Mpira wa Miguu (CAF) imeonesha Yanga itaanzia ugenini.
Azam FC ambao nao wameingia kwenye michuano hiyo wataanza nyumbani Uwanja Chamazi Complex dhidi ya APR ya Rwanda.
Kwa ratiba ya michezo mingine:http://>https://www.cafonline.com/caf-champions-league/videos/totalenergies-caf-champions-league-202425-preliminary-draw/