Yanga yazipumulia Simba, Azam

DAR ES SALAAM: USHINDI wa mabao 3-2 iliyoupata Yanga leo dhidi ya Mashujaa kwenye Uwanja wa KMC, Kinondoni, Dar es Salaam umerudisha vita ya miamba mitatu juu ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

 

Advertisement

Azam inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 33 kwa michezo 15, Simba inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 31 na Yanga inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 30 zote zikicheza michezo 12. Singida Black Stars nayo ina pointi 30 ipo nafasi ya nne ikizidiwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa na Yanga. Singida imecheza mechi 14.

Mabao ya Yanga katika mchezo wa leo yamefungwa na Prince Dube ikiwa ni hat-trick ya kwanza kufungwa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/25. Mabao ya Mashujaa yamefungwa na David Ulomi na Idrisa Stambuli