Zaidi ya milioni 450 kutekeleza miradi ya afya Longido

ZAIDI ya Sh milioni 450 zimepelekwa katika Jimbo la Longido mkoani Arusha kumalizia miradi ya afya ili kuwaondolea usumbufu wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma za matibabu.

Naibu Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Longido, Dk Steven Kiruswa amesema hayo katika mikutano ya hadhara iliyofanyika Tarafa ya Longido kata ya Kimokowa na Namanga na kuongeza kuwa serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inawajali na kuwathamini wananchi wa Longido.

Dk Kiruswa amesema fedha hizo ni maalumu ambazo zimetolewa na serikali nje ya bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 zimelenga sekta ya afya kumalizia ujenzi wa zahanati na vituo vya afya katika baadhi ya kata wilayani Longido.

Amesema kuna kata vituo vya afya vilianza kujengwa kwa michango ya wananchi na mchango wake binafsi mbunge lakini miradi hiyo haikukamilika kutokana na juhudi za mbunge kuomba fedha serikali na serikali imeona umuhimu wa kutoa fedha hizo ili kumalizia miradi hiyo.

Mbunge Kiruswa amesema kata ya Mundarara zilipelekwa Sh milioni 250 kwa ajili ya kumalizia zahanati ya kisasa iliyojengwa katika kata hiyo yenye msongamano mkubwa wa watu kwa kuwa kata ya Mundarara imebarikiwa kuwa na madini ya Ruby hivyo kuna wananchi wengi kutoka maeneo mbalimbali ya nje ya Wilaya ya Longido hivyo kuwa na uhitaji mkubwa wa zahanati.

Amesema katika tarafa ya Ketumbeine kijiji cha Losuruway zanahati ya kisasa imejengwa na imekamilika lakini ilikuwa haina nyumba vya daktari hivyo serikali ilitoa Sh milioni 45 kumalizia ujenzi wa nyumba hiyo sambamba na kata ya Loirienyito kituo cha afya kimepelekwa fedha Sh milioni 45 kumalizia ujenzi wa kituo hicho cha afya.

Naibu Waziri Kiruswa amesema kata ya Kimokowa tarafa ya Longido zimepelekwa Sh milioni 45 kuendeleza na kumalizia zanahati iliyojengwa katika kata hiyo sambamba za Sh milioni 30 zilizopelekwa kata ya Noondoto kijiji cha Ngusero kumalizia ujenzi za Kituo cha afya, Sh milioni 30 kupelekwa kijiji cha Naadale kumazilia ujenzi wa kituo cha afya.

Amesema katika fedha hizo pia Sh milioni 30 zimepelekwa katika kijiji cha Wosiwosi kilichopo tarafa ya Ketumbeini kumalizia ujenzi wa kituo cha afya ambapo awali wananchi na mbunge walianzisha ujenzi wa kituo hicho na serikali imewakumbuka na kutoa fedha kwa ajili ya umaliziaji wa kituo hicho.

Dk Kiruswa amesema kuwa wananchi wa jimbo hilo wanamshukuru sana Rais kwa uamuzi wake wa kutoa fedha kwa ajili ya umaziaji wa zahanati na vituo vya afya katika baadhi ya kata na kusema kuwa huo ni uamuzi ulioshukuruliwa kwa akiasi kikubwa na wananchi wa Jimbo la Longido.

Mbunge huyo yuko katika ziara ya siku nne katika Jimbo la Longido kueleza miradi iliyotelekezwa na serikali na mchango wake kama mbunge kwa wananchi wa Jimbo hilo na kueleza ahadi alizoahidi ambazo amezitekeleza kwa asilimia mia moja.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button