Zaidi ya watu 65 wauawa Sudan

SUDAN: TAKRIBAN watu 65 wameuawa na wengine zaidi ya 130 wamejeruhiwa kufuatia mapigano makali kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF (Rapid Support Forces).

Taarifa zinasema kuwa katika jimbo la Kordofan Kusini, watu 40 wameuawa na wengine 70 wamejeruhiwa kufuatia mashambulizi yaliyofanyika katika mji mkuu wa jimbo la Kadugli.

Mji huo, ambao unadhibitiwa na jeshi la Sudan, ulikuwa lengo kuu la shambulio hilo. Gavana wa jimbo la Kordofan Kusini, Mohamed Ibrahim, amekilaumu kundi la Sudan People’s Liberation Movement-North (SPLM-N), linaloongozwa na Abdel Aziz al-Hilu, kwa kuhusika na shambulio hilo.

Advertisement

SOMA: Sudan yalaani vikwazo vya Marekani dhidi ya Abdel Fattah

Mapigano makali pia yalishuhudiwa magharibi mwa Darfur, ambapo mashambulizi yalilenga mji mkuu wa Darfur Kusini, na kusababisha vifo vya watu 25 huku wengine 63 wakijeruhiwa.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *