MAMLAKA ya Mapato (TRA) imesema vikao na ziara wanazofanya kukutana na wafanyabiashara kuzungumzia changamoto zinazowakabili wafanyabiashara katika ulipaji kodi umechochea ulipaji kodi kwa hiari na kuifanya mamlaka hiyo kuvuka malengo ya ukusanyaji.
Kamishna wa upelelezi wa kodi (TRA), Hashim Ngoda amesema hayo walipofanyaza ziara mkoani Kigoma kuwatembelea, kuzungumza na kutoa zawadi kwa baadhi ya wafanyabiashara kutambua mchango wao na kuwa mabalozi kwa wengine katika suala zima ulipaji kodi kwa hiari.
Kamishna wa upelelezi wa kodi (TRA), Hashim Ngoda (wa pili kulia) akitoa zawadi kwa Mfanyabiashara wa mjini Kigoma Kilahumba Kivumo (kushoto) wakati maafisa wa mamlaka hiyo walipofanyaza ziara mkoani Kigoma kuwatembelea, kuzungumza na kutoa zawadi kwa baadhi ya wafanyabiashara kutambua mchango wao na kuwa mabalozi kwa wengine katika suala zima ulipaji kodi kwa hiari.
Ngoda akimwakilisha Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuf Mwenda amesema kuwa vikao mikutano na ziara hizo zimekuwa zikifurahiwa na wafanyabiashara na vimekuwa na matunda makubwa katika kukabiliana na uingizaji wa bidhaa za magendo na hali hiyo imefanya kuwepo kwa ongezeko kubwa la makusanyo hivyo kufikia na kuvuka lengo.
Akizungumza baada ya kupokea zawadi kutoka kwa Uongozi wa TRA Mkurugenzi wa Kampuni ya Falcon Marine, Mbaraka Mussa amesema kuwa ziara hizo zimekuwa Faraja kubwa kwao kuona namna TRA inavyowajali na kushughulikia matatizo yao ya kikodi.