“Zingatieni mifumo kutangaza zabuni”
KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Godfrey Mnzava amezitaka halmashauri na taasisi zote za serikali kuzingatia matumizi ya mifumo katika kutangaza zabuni na kufanya manunuzi ya umma ikiwa ni kutekeleza sheria ya manunuzi nchini.
Mnzava ametoa kauli hiyo leo akiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji Mwenge wa Uhuru ulipotembelea ,kuzindua na kukagua miradi ya maendeleo mkoani Kigoma.
Amesema matumizi ya mifumo katika kutangaza zabuni na kufanya manunuzi inasaidia katika kukabili rushwa, udanganyifu na kuweka uwazi wa matumnizi ya fedha katika utekelezaji wa miradi.
SOMA: Mwenge wa Uhuru wakagua miradi ya Sh Bil 5 Iramba
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru wakikagua barabara ya kiwango cha lami ya Stanley iliyojengwa na TARURA kwa gharama ya Sh Bilioni 1.7
SOMA: Mwenge wa Uhuru kukagua miradi ya Sh bilioni 1 Ukerewe
Amesema kuwa wakati huu ambao dunia imehamia kwenye mifumo ya mawasiliano ya Teknolojia ya Habari na mawasilinao matumizi ya mifumo kwa ajiili ya kuendesha shughuli za serikli kidijitali haliepukiki.
Akikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami iliyojengwa na wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA) yenye urefu wa kilometa 1.1 kiongozi huyo wambio za mwenge alisema kuwa utekelezaji wa miradi ya wananchi haina budi kuzingatia ubora na thamani ya fedha zilizotekeleza miradi hiyo ionekane.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa barabara hiyo Meneja wa TARURA Wilaya Kigoma, Elius Mutapima alisema kuwa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 1.1 imegharimu kiasi cha Sh bilioni 1.7 ambapo ujenzi wake umekamilika.