Zitto atahadharisha utitiri kampuni za hisa serikalini

ARUSHA: KIONGOZI wa Chama cha ACT – Wazalendo Zitto Kabwe ametahadharisha kasi ya baadhi ya Wizara kuunda kampuni kusimamia hisa za serikali katika kampuni binafsi akishauri utaratibu mpya wa kuanzishwa kampuni moja itakayo simamia hisa zote za serikali katika kampuni binafsi.

Serikali ina hisa kwenye kampuni binafsi 37 zenye thamani ya Sh trilioni 32.

Kwa mujibu wa Zitto serikali imekua ikianzisha kampuni tanzu kisimamia hisa pale inapokuwa na umiliki mdogo kwenye kampuni binafsi. 

Akitolea mfano Wizara ya Madini, Zitto amesema: “huko sasa kuna Twiga Minerals, Tembo na punde tutasiki Swala… Serikali ianzishe kampuni itakayo miliki hisa zote kwa niaba ya serikali katika taasisi binafsi.”

Zitto amesema Kampuni hiyo ikianzishwa iwe chini ya Msajili wa Hazina. Amesema utaratibu kama huo umefanyika katika nchini kama  Malaysia na umeonesha ufanis mkubwa.

Hata hivyo amesema kampuni hiyo ikianzishwa inaweza sajiliwa katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE).

Habari Zifananazo

Back to top button