20,000 wachukua fomu CCM

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema watia nia waliochukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi Ubunge, Udiwani na Uwakilishi kupitia chama hichi ni zaidi ya 20,000.
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amos Makalla ametoa taarifa hiyo leo Julai 3, 2025 Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mchakato wa ndani ya chama unaofuata baada ya kuhitisha uchukuaji fomu.
Makalla amesema waliojitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya majimbo ni 4,109 kati ya majimbo 272 yaliyopo, ambapo 3,585 ni kutoka Tanzania Bara na 524 kutoka Zanzibar.
Katika upande wa uwakilishi Zanzibar wamechukua wanachama 503, Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) 623, upande wa bara na ndani yake kuna watu 91 wa makundi maalumu na nane kutoka Zanzibar na Viti maalumu uwakilishi Zanzibar tisa ambao jumla ni 640.
Makalla amesema Umoja wa Vijana CCM(UVCCM) wamechukua 161 kati ya hao 154 kutoka Tanzania Bara na saba kwa upande wa Zanzibar. Jumuiya ya wazazi ni 62, kati ya hao, 55 kutoka bara na saba kutoka Zanzibar.
Pia amasema Idadi hiyo imefanya CCM kuwa na idadi ya jumla ya watu 5474 waliochukua fomu za kuwania nafasi ya ubunge na uwakilishi kutoka Tanzania bara na Zanzibar.
Makalla amesema katika Kata 3960 watia nia ni zaidi ya 15,000.