Ujenzi waiva kituo cha polisi Mchinga

LINDI: Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohammed Mahmoud amesema Serikali itaanza ujenzi wa kituo kipya cha Polisi cha Mchinga kwa lengo la kuboresha mazingira ya kazi kwa askari na kuongeza ubora wa huduma za usalama kwa Wananchi kufuatia ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika eneo hilo.

Akizungumza leo mara baada ya ukaguzi wa kituo hicho kilichopo Wilayani Mchinga mkoani Lindi, Naibu Waziri Ayoub amesema Serikali imechukua hatua hiyo baada ya kubaini kuwa kituo cha sasa hakikidhi mahitaji ya utoaji huduma bora kwa askari na wananchi.

Amebainisha kuwa ukuaji wa miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo mradi wa gesi asilia unaotarajiwa kuendelezwa katika ukanda huo, unalifanya eneo hilo kuhitaji miundombinu imara ya usalama ili kuendana na kasi ya maendeleo ya kiuchumi.

Vilevile, amesema kuwa kituo hicho kinatarajiwa kuwa cha Daraja C ambacho kwa wastani kinagharimu takribani Milioni 165.

Ambapo hatua za awali za ujenzi zinatarajiwa kuanza kwa kutumia fedha kiasi cha Sh milioni 50, huku juhudi zaidi zikiendelea kufanyika kuhakikisha upatikanaji wa fedha zilizobaki ili kukamilisha mradi wa kituo hicho.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button