ATCL yarejesha huduma Chato

DODOMA; SERIKALI imesema Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), itarejesha safari zake za ndege ya abiria kwenye Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita kuanzia Juni 2, 2026.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Mei 25, 2026 na Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Chato Kaskazini, Cornel Magembe aliyehoji bungeni ni lini serikali itarejesha safari za ndege Uwanja wa Ndege Chato mkoani Geita.

Naibu Waziri amesema tangu ATCL itangaze kurejesha huduma hizo kwa Uwanja wa Ndege wa Chato, muitikio wa wananchi kukata tiketi umekuwa mkubwa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button