Real Madrid yamtetea Zidane

MABINGWA wa kihistoria wa Ulaya Real MadridΒ wamesikitishwa na kauli isiyo ya kiungwana na iliyotafisiriwa kumkosea heshima ya Rais wa Shirikisho la soka la Ufaransa,Β Noel Le Graet, kumhusu Zinedine Zidane.
Baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar ziliibuka tetesi kuwa kiungo wa zamani wa Real Madrid na Ufaransa, Zinedine Zidane kuwa angeweza kuwa kocha wa Ufaransa au Brazil.
Tetesi za kuhusishwa na kuifundisha Brazil, Rais Noel Le Graet hakupendezeshwa nayo na aliposikia taarifa hizo alisema Β βπππ πππ ππππ πππππ ππ π©πππππ?Β π―ππππππππ ππππ πππ πππ, πππππππ πππππ π ππππππ πππππππππ! π°ππ πππππ ππ πππππ ππ πππππ ππ ππππ ππ πππππ, πππππππ ππππππ ππππππππ πππππππππππ πππππ.
βπ¨ππππππ πππππππππππ ππ ππππ πππ πππππ ππ ππππ ππ πππππ? π―πππππ, ππ ππππππππππππ ππππ ππππ ππππ.β aliongeza
Katika taarifa yao Real Madrid wameandika.
βZinedine Zidane,Β bingwa wa dunia na bingwa wa Ulaya akipigania jezi ya taifa lake, pamoja na mataji mengine mengi, anawakilisha tunu za mchezo huu na amethibitisha hilo katika maisha yake yote ya soka, kama mchezaji na kama kocha.β
βKauli ya Rais wa Shirikisho la soka Ufaransa haikubaliki hasa kwa mtu anayebeba uwakilishi kama wake, na inamdhalilisha mwenyewe, ukirejea pia alishawahi kutoa kauli kama hizo kwa nahodha wetu Karim Benzema, mshindi wa sasa wa Ballon d’Or, Ligi ya mataifa ya Ulaya akiwa na Ufaransa mwaka 2021 na mshindi mara tano wa ligi ya mabingwa Ulaya pamoja na mataji mengine mengi.β



