Dar City, JKT Stars hazikamatiki

KLABU ya mpira wa kikapu ya Dar City imeanza vyema mchezo wa robo fainali Ligi ya Kikapu mkoa wa Dar es Salaam kwa ushindi wa vikapu 79-45 dhidi ya Srelio katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa Don Bosco, Dar es Salaam.

Kwa upande wa wanawake JKT Stars imeshinda mchezo dhidi ya Polisi Stars kwa vikapu 78-53.

Michezo hiyo kwa washindi ni kama imetanguliza mguu mmoja hatua ya nusu fainali, wanahitajika kushinda michezo miwili kati ya mitatu wanayotakiwa kucheza ili kufuzu kwa uhakika.

SOMA: Tano zafuzu robo fainali kikapu Dar

Dar City na JKT Stars zote ni timu zilizomaliza hatua ya makundi zikiwa vinara na zote zimecheza na waliomaliza nafasi ya nane.

Katika michezo hiyo, wachezaji waliofanya vizuri ni Victor Mwoka wa Dar City aliyefunga pointi 21 na Sara Budodi wa JKT Stars aliyefunga pointi 14.

Timu hizo zitarudiana mchezo wa pili Oktoba 12 na matokeo yataamua atakayefuzu nusu fainali.

Michezo mingine itakayochezwa leo usiku ni Troncatti dhidi ya Pazi Queens na UDSM Outsiders dhidi ya Vijana.

Habari Zifananazo

Back to top button