KENYA: Mgomo wa madaktari kuanza 22 Desemba

KENYA : UMOJA wa Madaktari nchini Kenya umetangaza kuanza mgomo wa siku 21, utakaofanyika kuanzia tarehe 22 Desemba, ikiwa serikali haitotekeleza makubaliano ya utendaji kazi yaliyofikiwa mwaka 2017.
Takribani madaktari 4,000 kutoka hospitali za umma walifanya mgomo mnamo mwezi Machi mwaka huu, wakiilalamikia serikali kwa kushindwa kuwapatia kazi madaktari watarajiwa na kuboresha mazingira ya kazi katika hospitali za umma.
Mgomo huo ulisitishwa baada ya siku 56, baada ya serikali na madaktari kufikia makubaliano ya kutekeleza matakwa yao mnamo Mei 8, 2023.
Hata hivyo, hadi sasa, serikali haijatekeleza ahadi zilizofikiwa katika makubaliano hayo, na madaktari wameendelea kulalamika kuhusu utendaji wa kazi.
Baadhi yao wanadai kutolipwa mishahara yao licha ya kutoa huduma kwa mwaka mmoja bila ya kupata leseni. SOMA: Madaktari wagoma wakidai mazingira bora ya kazi
Ikiwa serikali haitatekeleza makubaliano hayo kabla ya mgomo kuanza, madaktari wamesema wataendelea na hatua hiyo, jambo linaloweza kuathiri huduma za afya kwa wananchi.



