Nyuki kung’ata au ni Azam kulamba asali leo?
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendeleo leo kwa michezo miwili kupigwa Tabora na Manyara.
Mkoani Tabora, wenyeji Tabora United #nyukiwatabora itawakaribisha wanalambalamba, Azam kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
SOMA: Tabora United wamtwisha mzigo kocha mpya
Azam inaongoza katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 30 baada ya michezo 13 wakati Tabora United ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 21.
Kwingineko ‘wanamangushi’ Coastal Union itakuwa mgeni wa Fountain Gate kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Babati mkoa wa Manyara.
Fountain Gate inashika nafasi ya nane ikiwa na pointi 17 baada ya michezo 12 wakati Coastal Union ni ya tisa ikiwa na pointi 16 baada ya michezo 13.



