INEC yafuta vituo 292, yatengua wagombea saba

TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imefuta vituo 292 vya kupigia kura.

INEC pia imetengua uteuzi wa wagombea udiwani saba wa maeneo ya uchaguzi yaliyofutwa baada ya maeneo hayo kuwa tengefu kwa ajili ya makazi ya wakimbizi.

Taarifa ya Mwenyekiti wa INEC, Jaji Jacobs Mwambegele imeeleza uamuzi huo umefanyika baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kuyatangaza maeneo ya Ulyankulu, Wilaya ya Kaliua Tabora, Katumba, Wilaya ya Mpanda na Mishamo, Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi kuwa maeneo tengefu kwa ajili ya makazi ya wakimbizi.

Alisema pia ni baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa kutoa amri ya marekebisho ya amri ya mgawanyo wa maeneo ya utawala katika serikali za mitaa ya mwaka 2025 kwa kuzifuta kata 10 za Litapunga, Kanoge, Katumba na vijiji viwili vya Ikolongo na Ndurumo vya Kata ya Mtapenda iliyopo Wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi.

Jaji Mwambegele alizitaja kata nyingine kuwa ni Mishamo, Ilangu, Bulamata na Ipwaga zilizopo Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi na kata za Milambo, Igombemkulu na Kanindo zilizopo Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora.

‘’Kwa kuwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), amezifuta kata tajwa, Tume imewatengua wagombea udiwani saba katika kata saba ambazo ni miongoni mwa kata kumi zilizofutwa kwa kuzingatia masharti ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za mwaka 2025,’’ alisema Jaji Mwambegele.

Aliwataja wagombea waliotenguliwa kuwa wagombea udiwani ni wa Kata ya Kanonge, Salehe Msompola, Kata ya Katumba, Elius Elia, Mohamed Asenga wa Kata ya Litapunga na Nicas Nibengo wa Kata ya Bulamata na wote walikuwa wagombea kupitia Chama Cha mapinduzi (CCM).

Wagombea wengine waliotenguliwa ni Rehani Sokota wa Kata ya Ipwaga, Juma Kansimba wa Kata ya Mishamo na Sadick Mathew wa Kata ya Ilangu (wote ni wa CCM).

Alieleza kuwa hata hivyo kata tatu zilizofutwa za Wilaya ya Kaliua hazijafanya uteuzi wa wagombea wao wa udiwani, kata hizo ni Milambo, Igombemkulu na Kanindo.

“Kutokana na mabadiliko hayo, Tume imevifuta vituo 292 vya kupigia kura vilivyokuwa kwenye kata zilizofutwa na kwa kushauriana na watendaji wa uchaguzi wa maeneo husika na kwa kuzingatia ukaribu wa maeneo wanayoweza kufika wapigakura, Tume imeanzisha vituo 292 vya kupigia kura katika maeneo jirani na kata zilizofutwa ili kuwawezesha wapigakura kutoka maeneo yaliyofutwa kwenda kupiga kura,’’ alisema.

Alisema jumla ya wapigakura 106,288 waliokuwa kwenye vituo vilivyofutwa wamehamishiwa kwenye vituo 292 vya kupigia kura vilivyoanzishwa katika kata za Mtapenda, Uruwira, Nsimbo na Ugala zilizopo Wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi.

Aliongeza kuwa kata nyingine walizohamishiwa ni Sasu, Ilege, Uyowa, Makingi na Silambo zilizopo Kaliua, Mkoa wa Tabora na Kata ya Tongwe iliyopo Tanganyika mkoani Katavi.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button