Dk Biteko ahitimisha kampeni Bukombe

GEITA; NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukombe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk Dotto Biteko amehitimisha rasmi kampeni za uchaguzi wa chama hicho katika jimbo la Bukombe mkoani Geita.
Dk Biteko amehitimisha kampeni hizo katika mkutano uliofanyika Oktoba 27, 2025 katika viwanja vya Kata ya Igulwa wilayani Bukombe, ambapo ametumia nafasi hiyo kusisitiza ushiriki wa makundi yote katika uchaguzi mkuu.

Dk Biteko amesema makundi yote kwa kuzingatia vigezo vya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), yana nafasi ya kuhakikisha yanaitikia na kushiriki kikamilifu upigaji kura katika uchaguzi mkuu Oktoba 29, 2025
Amesema mchakato wa uchaguzi unagusa maisha ya makundi yote ya kijamii, hivyo kila mtu anao wajibu na umuhimu wa kushiriki.
Amewaomba wakazi wa Bukombe kujitokeza kwa uwingi kupiga kura ili kutenegeneza historia ya ushindi wa kihistoria kwa CCM na kuifanya Bukombe kuonesha mfano wa kuigwa Tanzania.

“Oktoba 29, 2025 siyo siku ya mzaha, ni siku ya watu wote kuacha shughuli zote twende tukapige kura, nataka nione upigaji wa kura Wilaya ya Bukombe unakua wa maana sana,” amesema.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com