ACT Wazalendo yatangaza wagombea ubunge11 Moro

MOROGORO : CHAMA cha ACT Wazalendo Mkoa wa Morogoro kimetangaza wagombea wa nafasi ya ubunge kwenye majimbo 11 ya mkoa huo kwa ajili ya kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu.

Katibu wa ACT Wazalendo mkoa huo, Mohamed Mnamata alisema hayo juzi kuwa majimbo yote 11 yamepata wagombea wa ubunge na kwenye kata zote za mkoa huo na kupata wagombea mahiri, wenye sifa na kukubalika kwenye jamii katika maeneo yao kwa nafasi ya ubunge na udiwani mkoani humo na baadhi ya wateule wa udiwani wameanza kuchukua fomu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa wasimamizi wa ngazi ya kata kuanzia Agosti 14, mwaka huu.

Kwa upande wa ubunge kupitia chama hicho Jimbo la Morogoro Mjini wagombea wawili wametia nia ambao ni Juma Tembo na Jamal Hamza. “Juma Tembo katika siku zilizopita aliwahi kuwa Chadema na pia kuwa diwani kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro uchaguzi wa 2015 na hivi sasa amejunga na ACT Wazalendo na kutia nia ya kuwania ubunge, tutaingia kwenye mchujo anatakayechaguliwa ndiye atapeperusha bendera ya chama,” alisema.

Mnamata aliwataja wengine na majimbo yao katika mabano ni Hamis Mwinyimsanga (Morogoro Kusini Mashariki), Nassor Athuman (Morogoro Kusini), Hussein Maige (Kilombero), Ally Matwiku (Ulanga) na Apolinary Ngonga (Mlimba). SOMA : Wananchi Morogoro wahimizwa kushiriki uchaguzi mitaa

Wengine ni Issaya Makuya (Gairo), Kassela Mdachi (Mikumi), Mbaruku Hassan (Kilosa), Kashikashi Saimanga (Mvomero) na Agnes Chapoteli (Malinyi). Kuhusu wagombea wa udiwani Jimbo la Morogoro Mjini alisema wamesimamisha wagombea kwenye kata 17 kati ya 29 zilizopo Manispaa ya Morogoro na wameshachukua fomu INEC kwa wasimamizi wa ngazi ya kata .

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button