Adaiwa kuiba ng’ombe, kunyonga watoto waliokuwa wakichunga

MBEYA; JESHI la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia mkazi wa kijiji cha Madundasi kilichopo wilayani Mbarali, Doto Lubongeja kwa tuhuma za mauaji ya watoto watatu wa familia moja kwa kuwanyonga na kamba shingoni.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya,Wilbert Siwa, amewataja watoto waliouawa ni Petro Amosi(8), Samu Amosi(6) na Nkamba Amosi(4) wote wakazi wa Kijiji cha Madundasi.

Amesema tukio hilo lilitokea  jana Januari 15, 2026 kijijini hapo, ambapo mtuhumiwa aliua watoto hao baada ya kuwakuta peke yao wakichunga ng’ombe jirani na nyumbani kwao.

Amesema baada ya kutekeleza mauaji hayo aliiba ng’ombe 15 kisha kuziswaga na kuzificha nyumbani kwa mjomba wake aitwaye Masoda Kulwa, anayeishi Kijiji cha Madundasi B na kuanza kutafuta mteja, ambapo aliuza ng’ombe hao na kupata fedha Sh milioni 5.1

Alisema kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa  lilianza msako mkali na kufanikiwa kumkamata  Doto Lubongeja pamoja na Masoda Kulwa, ambaye walishirikiana kuuza ng’ombe hao.

Alisema kupitia msako huo askari hao walifanikiwa kupata ng’ombe wote 15 waliokuwa wameibwa pamoja na fedha zilizopatikana kwa mauzo ya ng’ombe hao

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button