Ahmadiyya waipongeza serikali kudumisha amani

MOROGORO: JUMUIYA ya Waislamu wa Ahmadiyya Tanzania imeisifu Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kusimamia amani, kuleta utulivu,  kujali misingi ya haki na huruma kwa binadamu wote.

Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya hiyo nchini, Sheikh Khawaja Muzaffar Ahmad amesema hayo mjini Morogoro kwenye maadhimisho ya siku ya kuazishwa Jumuiya hiyo mwaka 1889.

Ahmad amesema  jumuiya hiyo ina sera ya kutii wa serikali yoyote iliyopo madarakani na sera ya kuunga mkono mikakati yoyote ambayo inawekwa na serikali katika kuleta maendeleo na ustawi wa jamii.

“Jumuiya yetu inaisifu Serikali inayoongozwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kulinda na kudumia amani …hii ni sifa kubwa wa Tanzania, serikali yetu na viongozi wetu” amesema.

Ameomba hali ya amani iendelee kudumishwa ikiwa na kupata viongozi wa serikali ambao wanajali amani ya nchi yetu ,kujali ubinadamu viongozi wanaoheshimu misingi ya haki na huruma kwa binadamu wote.

Aliipongeza serikali kwa kuwa na sera ya kutokuwa na dini isipo kuwa watu wake ndiyo wenye dini.

Ahmad amesema Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya inayo msimamo wazi ya kwamba ubinadamu ni jambo la kwanza kuliko mengine yoyote yale na hivyo kubaki katika msingi huo.

“Ombi langu na la Jumuiya ni kwamba viongizi wa ngazi mbalimbali wawe mstari wa mbele kuwasaidia watu wa nyonge “ amesema

Kwa upande wake Mkuu Wilaya ya Morogoro, Mussa Kilakala aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo aliipongeza Jumuiya hiyo kwa kusaidia utoaji wa huduma za kijamii hususani sekta ya elimu, maji , afya na kutoa huduma ya kiroho.

Awali,Naibu Amiri wa Jumuiya hiyo nchini ,Sheikh Abid Mahmood Bhatti ,amesema maadhimisho hayo jumuiya hiyo iliwezesha kugawa vyakula ambao ni mchele na unga wa sembe takribani tani 1.5 kwa kaya zaidi ya 150 zenye uhitaji kwenye mitaa tisa ya kata ya Kihonda Maghorofani, Manispaa ya Morogoro.

Sheikh Bhatti aliitaja kaya hizo ni kutoka mitaa ya Ngerengere, Kitata, Msamvu B, Airport ,Kihonda Maghorofani “A” na “B” , Godes , Bima na Mbuyuni kwa ajili ya mahitaji yao kwenye mwezi mtukufu wa Ramadhani, ambayo hufanyika kila mwaka.

Naibu Amiri wa Jumuiya hiyo amesema lengo ni kuunga mkono wito wa Serikali inayohimiza mashirika, taasisi,na watu binafsi kutoa misaada kwa jamii yenye uhitaji.

Mmoja wa wahitaji ,Catherine Ngongi ameishukuru Jumuiya hiyo kwa upendo wa kuwakumbuka walengwa wa dini tofauti wa mitaa za Kata ya Kihonda Maghorofani kuwapatia chakula kwa ajili ya Eid inayokuja na ameomba madhehebu ya dini nyingine wainge mfano huo.

Habari Zifananazo

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button