Ajali basi, coaster yaua 37 Same

WATU 37 wamepoteza maisha na wengine 29 kujeruhiwa katika ajali mbaya ya barabarani iliyotokea jioni ya Juni 28, 2025, katika eneo la Sabasaba, Kata ya Same, wilayani Same, mkoani Kilimanjaro.

Ajali hiyo ilihusisha basi la kampuni ya Channel One lililokuwa likitokea Moshi kwenda Tanga na basi dogo aina ya Coaster lililokuwa likitokea Same, ambapo magari hayo yaligongana uso kwa uso na kushika moto.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, amesema ajali hiyo ni tukio la majonzi makubwa ambalo halijawahi kushuhudiwa katika mkoa huu, akifafanua kuwa majeruhi 24 wamelazwa katika Hospitali ya Mji Same, huku watano wakiwa katika Hospitali ya Mawenzi na KCMC kwa matibabu zaidi.

Ameongeza kuwa, kutokana na hali ya miili ya marehemu kuungua vibaya, serikali imeanza taratibu za uchunguzi wa vinasaba (DNA) kusaidia kuwatambua marehemu, huku wananchi wakihimizwa kufuatilia taarifa za wapendwa wao waliopotea ili kusaidia zoezi hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro ameeleza kuwa chanzo cha ajali ni kupasuka kwa tairi la mbele la basi la Channel One, lililosababisha basi hilo kupoteza mwelekeo na kugongana na Coaster kabla ya magari hayo kushika moto.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button