Ancelotti aitaka saini ya Enzo kwa udi na uvumba

Kiungo wa Chelsea, Enzo Fernandez.

TETESI za usajili zinasema Real Madrid ipo tayari kutoa Aurélien Tchouaméni kwa Chelsea kama sehemu ya makubaliano ya kumsajili kiungo Enzo Fernandez, ambaye anahitajika binafsi na kocha Carlo Ancelotti. (Fichajes – Spain)

Kiungo mkabaji wa PSG, Aurélien Tchouaméni.

Maofisa katika klabu ya Real Madrid wamekuwa na ongezeko la wasiwasi kuhusu kiwango cha Tchouameni na sasa wanajiandaa kusikiliza ofa kwa ajili ya kumsajili mfaransa hiyo. (Jorge C Picon)

Barcelona inapanga kumsajili golikipa mpya majira yajayo ya kiangazi na imemuangazia mlinda lango wa Porto, Diogo Costa. (Relevo – Spain)

Advertisement

SOMA: Madrid, City usiku wa kisasi

Chelsea pia imeonesha nia kwa Costa lakini inakabiliwa na ushindani kutoka Bayern Munich, ambayo inaweza kuhitaji saini ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno kwa sababu kipa namba moja wa miamba hiyo ya Bavaria, Manuel Neuer anafikiria kustaafu mwisho wa msimu huu. (CaughtOffside)

Iwapo Porto itamuuza Costa, huenda ikamsajili Filip Jorgensen wa Chelsea kuziba pengo lake. (Fichajes – Spain)

Brentford itadai zaidi ya pauni milioni 60 ili kumuuza mshambuliaji Bryan Mbeumo Januari 2025, wakijaribu kuzima nia ya Arsenal. (Football Insider)

Liverpool, Manchester City na Real Madrid zote tatu zimeelezea nia ya kumsajili beki wa kulia wa Paris Saint-Germain, Achraf Hakimi. (Fichajes – Spain)