DAR ES SALAAM : WATAALAMU wa afya nchini wamesema asilimia 64 ya watoto nchini ndio wanaonyonya maziwa ya mama hivyo jamii imetakiwa kuungana kwa pamoja katika kutoa elimu kuhusiana na umuhimu wa unyonyeshaji wa watoto kwa ufanisi
Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Daktari bingwa wa watotokutoka hospitali ya Aga Khan,Dk. Mariam Noorani katika maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani.
Dk. Mariam ameshauri serikali na taasisi zingine kufanya maboresho katika maeneo ya kazi kwa kuweka sehemu maalum za kunyonyesha.
Kuhusu suala la lishe bora kwa mama anayenyonyesha,Mtaalamu wa lishe kutoka hospitali ya Aga Khan Luiza Tumaini amesema ni muhimu kuzingatia matumizi ya vyakula vinavyoongeza virutubisho muhimu kwa maziwa ya mama ikiwemo matunda mbogamboga na vyakula vyenye protini ili kulinda madini kwenye mwili na maziwa ya mama.
SOMA: Washauri ujenzi vyumba vya kunyonyeshea
Kwa upande wake mtaalamu wa lishe na masuala ya unyonyshaji Idda Katigula amesisitiza umuhimu wa utunzaji wa maziwa ya mama kabla ya matumizi.
Wiki ya unyonyeshaji duniani huadhimishwa kila Agosti 1 mpaka 8 kila mwaka ambapo kwa mwaka huu imebebwa na kauli mbiu isemayo “kutatua changamoto na kufanikisha unyonyshaji kwa wote duniani”