Bajeti ya utafiti yaongezwa maradufu

SERIKALI imeongeza fedha za utafi ti kutoka Sh bilioni tatu hadi kufi kia bilioni tisa kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 kwa ajili ya kuendeleza sayansi, teknolojia na ubunifu utakaowezesha kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga alisema hayo hivi karibuni akizindua kigoda cha Oliver Tambo katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), mkoani Morogoro. Kipanga alisema mwaka wa fedha wa 2021/2022, serikali ilitenga Sh bilioni tatu katika bajeti yake na kwa kutambua umuhimu wa utafiti imeongeza bajeti mara mbili zaidi kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Alisema tafiti zinazofanyika, matokeo yake yanatumika kutatua changamoto ambazo jamii inazikabili, hivyo imekuwa ikiongeza bajeti hiyo kukidhi mahitaji ya kitafiti. Naibu waziri alisema serikali inaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kisasa vya utafiti na kwamba imepata zaidi ya dola za Marekani milioni 425 sawa na Sh bilioni 972 ambazo ni mkopo wa miaka mitano.

“Lengo la serikali ni kuona tafiti zinazofanyika zinatoa mchango wa kusaidia kutatua magonjwa ya binadamu na wanyama ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza,” alisema Kipanga.

Mwenyekiti wa Kigoda cha Oliver Tambo kutoka Chuo Kikuu SUA, Profesa Gerald Misinzo alisema mpango huo umejengwa kutokana na kazi ya Oliver Tambo, kiongozi mashuhuri wa Afrika Kusini aliyebobea katika historia ya elimu ya sayansi, aliyeamini mageuzi kupitia utoaji elimu, ushirikiano na mshikamano wa mataifa Afrika.

Alisema kwa mara ya kwanza, mpango huo ulitangazwa mwaka 2017 katika maadhimisho ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa kiongozi huyo ambaye alipambania ukombozi wa Afrika na kuongoza Chama cha African National Congress (ANC) wakati akiwa uhamishoni nje ya nchi.

Habari Zifananazo

Back to top button