Bamba wa PSG afariki dunia

SOL Bamba, beki wa zamani wa Leeds United, Leicester City, Cardiff City na Hibernian, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 39.

Beki huyo wa kati wa Ivory Coast, ambaye alianza maisha yake ya soka akiwa na Paris St-Germain na pia alichezea Dunfermline na Middlesbrough, alikuwa sehemu ya kikosi cha Cardiff  kilichopanda Ligi Kuu mwaka 2018.

SOMA: Mshambuliaji Ufaransa afariki dunia

Taarifa kutoka timu ya Adanaspor alipokuwa akifanya kazi ilisema: “Mkurugenzi wetu wa ufundi Souleymane Bamba, ambaye aliugua kabla ya mechi dhidi ya Manisa siku ya Ijumaa, alipelekwa hospitalini na kwa bahati mbaya akapoteza vita vyake vya maisha huko. Tunatoa pole kwa familia yake na jamii yetu.”

SOMA: Nyota wa zamani Brazil afariki dunia

Klabu ya Cardiff imepokea habari hizo kwa huzuni ambapo katika taarifa yao wameeleza: “Huzuni kubwa zaidi”, ikimtaja Bamba kama “gwiji wa klabu” na kuongeza: “Kama mchezaji na kocha, athari ya Sol kwa klabu yetu ya soka ilikuwa isiyo na kipimo. Alikuwa shujaa kwetu sote.”

Habari Zifananazo

Back to top button