Benjamini Mkapa yajivunia mambo 15 kuanzishwa kwake

DODOMA: MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Profesa Abel Makubi ameeleza mafanikio makubwa 15 ya taasisi hiyo katika miaka 10 tangu ianzishwe.

Mojawapo ni kupunguza rufaa kwa wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya hospitali hiyo kwa asilimia 85 tangu hospitali hiyo izinduliwe Oktoba 13, 2015.

Alikuwa akiizungumzia mafanikio ya hospitali hiyo katika kipindi hiki cha maadhimisho ya miaka 10 ya hospitali hiyo yatakayohitimishwa Februari 26 mwakani. Profesa Makubi alisema hospitali hiyo imejiimarisha pia kifedha, kwani ina uwezo wa kununua dawa, vitendanishi na vifaatiba kwa asilimia 95 kutoka asilimia 30 wa mwaka 2016.

“BMH inatoa huduma bora na zenye kutumia teknolojia ya kisasa,” alisema. Profesa Makubi alisema BMH imeimarisha mawasiliano ya umma na utoaji wa elimu ya kinga na magonjwa kwa wananchi katika maeneo mbalimbali.

Pia, imepanua ushirikiano na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi. Profesa Makubi alisema BMH inaendelea kwa kasi kufanya utafiti wa tiba kwa kushirikiana na taasisi nyingine za ndani na nje ya nchi.

BMH inaendelea kutoa huduma za kibingwa kama Mkoba na Tembezi katika mikoa na maeneo ya pembezoni mwa mkoa, kanda ya kati na nchi. Vilevile, imeanzisha huduma za ubingwa wa juu za dharura na wagonjwa mahututi wa kawaida. Profesa Makubi alisema BMH imeanzisha chuo cha mafunzo ya diploma za afya na kituo cha mafunzo ya huduma za dharura.

Hata hivyo, imenunua vifaa vya kisasa vya uchunguzi kama CT-Scan, MRI na vya maabara ya kawaida na maabara ya moyo. Hospitali hiyo imeongeza idadi ya watumishi kutoka 22 wakati hospitali ikianza hadi kufikia wtumishi 967 mwaka 2024 na kuwaendeleza kwa kuwapa mafunzo.

BMH imesimika na kuendesha mtambo wa kuzalisha hewa ya oksijeni wenye uwezo wa kuzalisha mitungi ya gesi 400 kwa siku. Profesa Makubi alisema BMH imefanya upanuzi wa miundombinu ya huduma kwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa jengo la tiba za saratani, ikiwemo mionzi na saratani wenye thamani ya Sh bilioni 30.9.

Wakati huo huo, imeanzisha huduma ya upasuaji wa kisasa wa matundu kwa wagonjwa wenye mawe kwenye figo na njia ya mkojo. Pia, imeanzisha huduma za ubingwa wa juu kama upandikizaji figo, upandikizaji wa uloto na upasuaji wa ubongo na mifupa, upasuaji wa koo, pua, masikio, macho na kusafisha figo

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Single Mom Reveals How She Earns $89k/Yr Working 10 Hrs/Week From Home. Tired of paycheck-to-paycheck living? Meet Kelly from New York—a regular mom who cracked the code to recession-proof income without selling a thing! Now,Big thanks …
    .
    Here is I started____________________ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button