Bil 100/- kupeleka umeme vijijini Kigoma

WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) imesema kuwa  zaidi ya Sh Bilioni 100 zitatumjka kutekeleza miradi ya kupeleka umeme vijijini katika Mkoa wa Kigoma mpango unaoendelenga kuboresha shughuli za kiuchumi za wananchi wa vijijini mkoani humo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu amesema hayo baada ya kukamilisha ziara ya wilaya ya uvinza na manispaa ya Kigoma Ujiji  Bodi hiyo kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kupeleka umeme vijijini.

Kutokana na kiasi kikubwa cha fedha kinachotolewa na serikali kutekeleza miradi hiyo Meja Jenerali Kingu amesema kuwa ni lazima wakandarasi waliopewa kazi ya miradi hiyo wanatekeleza majukumu yao kulingana na mikataba na hakutakuwa na muda wa nyongeza kwa wakandarasi wanaochelewa miradi.

SOMA: EU yaweka nguvu miradi REA

Akizungumza katika ziara hiyo Mkurugenzi Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Balozi Radhia Msuya amesema kuwa ziara hiyo ni muendelezo wa ziara za bodi hiyo kuhakikisha inatembelea miradi inayosimamiwa na REA ili kuona miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kubadilisha hali za wananchi wa vijijini kama ilivyo dhamira ya serikali.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidi alisema kuwa katika mkoa wa Kigoma jumla ya Vijiji 279 kati ya Vijiji 306 tayari vimeunganishwa na nishati ya umeme na kusisitiza kuwa safari ya kupeleka umeme katika Vitongoji imeanza ambapo vitongoji 595 vinaendelea na utekelezaji wa mradi huo huku Katika vitongoji 1849 vilivyopo  Mkoa wa Kigoma vitongoji 1370 tayari vimeshapata umeme.

SOMA: Wakazi wa Mwanza wachangamkie fursa REA

Habari Zifananazo

Back to top button