Bima ya afya kujumuisha makundi matano

SHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote ya Mwaka 2023 imeeleza mfumo wa bima ya afya kwa wote utajumuisha makundi matano. Kifungu cha sita cha sheria hiyo itakayotumika Tanzania Bara kimetaja makundi hayo ni waajiri na waajiriwa katika sekta ya umma na sekta rasmi binafsi na watu walioko katika sekta isiyo rasmi.
Wengine ni skimu za bima ya afya; watu wasio na uwezo; vituo vya kutolea huduma za afya; na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA). Kifungu cha 5 (1) cha sheria hiyo kimeeleza bima ya afya itakuwa ni ya lazima kwa watu wote. “Kwa kuzingatia masharti ya sheria hii, kila mtu anapaswa kujiunga na skimu ya bima ya afya ili kuhakikisha anapata huduma za afya.
Kila mwajiri atatakiwa kumchangia mwajiriwa wake katika skimu ya bima ya afya kiwango cha uchangiaji kwa kuzingatia masharti ya sheria hii,” imeeleza sheria.Imeongeza: “Wageni wote wenye umri wa miaka 18 au zaidi wanaoingia nchini na kukaa zaidi ya siku thelathini ambao hawana bima ya afya inayotambulika nchini watapaswa kujiunga na bima ya afya kwa mujibu wa sheria hii”.
Sheria hiyo ina lengo la kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wote kupitia mfumo wa bima ya afya na kuweka mfumo wa ushiriki katika skimu za bima ya afya kwa raia na wakazi wote. “Mamlaka ya Udhibiti wa bima iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Bima itakuwa ndiyo mamlaka ya udhibiti wa huduma za bima ya afya,” imeeleza sheria hiyo.
Kifungu cha saba cha sheria hiyo kimeeleza TIRA itakuwa na wajibu wa kusajili skimu za bima ya afya na kuhakikisha bima za afya zinatoa kitita cha mafao ya huduma muhimu kwa mujibu wa sheria hii. SOMA: Bima ya Afya kwa Wote kutibu figo, moyo
Kwa kuzingatia sheria hiyo pia TIRA itakuwa na majukumu ya kuhakikisha huduma za bima zinazotolewa zinaendana na viwango vya michango; kutoa miongozo ya malipo kwa watoa huduma na kutoa miongozo ya uendeshaji wenye ufanisi na tija katika usimamizi wa skimu za bima ya afya.
Pia, mamlaka hiyo itapaswa kuhakikisha skimu ya bima ya afya ina ukwasi na akiba kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na kutunza kanzidata ya vituo vya kutolea huduma za afya vilivyoingia mikataba na skimu za bima ya afya. Sheria hiyo pia inaitaka TIRA ifanye ukaguzi wa skimu za bima ya afya; iweke miongozo kuhusu usajili wa wanachama katika skimu za bima ya afya; iombe au kuitisha taarifa yoyote itakayoihitaji.
TIRA pia itapaswa ifanye tafiti na uvumbuzi kwa lengo la kuendeleza ufanisi na uendelevu wa mfumo wa bima ya afya kwa wote na itekeleze jukumu lingine lolote kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa sheria hiyo. Kifungu cha nane sheria hiyo kimeeleza huduma za bima ya afya kwa wote zitatolewa na skimu binafsi. “Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ulioanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mfuko wa Taifa wa utekelezaji bora wa sheria hiyo.
Kifungu cha nane sheria hiyo kimeeleza huduma za bima ya afya kwa wote zitatolewa na skimu binafsi. “Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ulioanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya utatambulika kama skimu ya bima ya afya ya umma,” imeeleza sheria. Imeongeza: “Mtu atakuwa na sifa ya kusajiliwa kuwa skimu ya bima ya afya ya binafsi baada ya kutimiza masharti kama yatakavyoainishwa katika kanuni chini ya sheria hii”




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com