Boda boda kupewa elimu ajali za barabarani

SHIRIKA la Msalaba Mwekundu (TRCS) kwa kushirikiana na Kampuni ya Breweries Limited imezinduzi wa mpango wa mafunzo kwa waendesha piki piki kwa lengo kuwapa elimu ya kupunguza ajali.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Shirika (TRCS) Reginald Mhango amesema umuhimu wa mpango huo umekuja baada ya kuona ongezeko la ajali zinazohusisha pikipiki linahitaji utatuzi wa haraka.

Advertisement

“Mradi huu unalenga kushughulikia changamoto hizi kupitia elimu na mafunzo ya kina, hatimaye kupunguza vifo na majeraha, kuongeza uelewa ili kuimarisha uelewa wa waendesha pikipiki kuhusu sheria za usalama barabarani na mazoea salama ya kuendesha kwa 50% ndani ya mwaka wa kwanza,”

SOMA: Marufuku bodaboda kuingilia misafara ya viongozi

“Kupunguza ajali, kupunguza ajali na vifo vinavyohusisha pikipiki kwa 30% ndani ya miaka mitatu. kushirikisha waendesha pikipiki, Kuwashirikisha angalau waendesha pikipiki 10,000 nchini Tanzania katika mpango wa mafunzo ndani ya miaka miwili ya kwanza,” amesema Mhango.

“Ili kufikia malengo haya, mradi utashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo mamlaka za serikali za mitaa, vyama vya waendesha pikipiki, vikosi vya polisi (Kitengo cha Usalama Barabarani), Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), na viongozi wa jamii,” ameongeza.

SOMA: Bodaboda: tupo tayari kulipa kodi

Mkurugenzi Mtendaji wa Breweries Limited, Michelle Kilpin amesema amesema kampuni hiyo inaunga mkono lengo la maendeleo endelevu ya umoja wa kimataifa (SDG) la kupunguza idadi ya vifo na majeraha yatokanayo na ajali za barabarani ifikapo 2030.