Bodi ya filamu yamwita Wema Sepetu

DAR ES SALAAM : BODI ya Filamu Tanzania imemuita muigizaji maarufu Wema Sepetu, almaarufu Chimama, kufika katika ofisi zao zilizopo Kivukoni, Dar es Salaam, Alhamisi Mei 22, 2025, saa nne asubuhi kwa mahojiano maalum.

Kupitia taarifa iliyowekwa kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram, Bodi hiyo imetoa wito huo kufuatia picha zilizosambaa mitandaoni zikimuonesha Wema akiwa amevaa mavazi yanayoelezwa kukiuka maadili na staha ya jamii ya Kitanzania.

 

Bodi ya Filamu imesisitiza kuwa ina wajibu wa kusimamia maadili na nidhamu katika sekta ya filamu, na haitasita kuchukua hatua dhidi ya mienendo yoyote inayohatarisha taswira ya tasnia na maadili ya taifa.

Aidha, imewahimiza wadau wote wa filamu nchini kuendelea kuwa mfano wa kuigwa katika kazi zao na maisha ya kila siku kwa kudumisha maadili, utamaduni na heshima ya taifa.

SOMA: Wasanii wajitokeza kupima magonjwa ya moyo Dar

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button