CCM kuzindua Ilani ya uchaguzi mwezi huu

MKUTANO Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa utafanyika Mei 29 na 30 jijini Dodoma ambao utatumika kuzindua Ilani ya Uchaguzi.

Taarifa ya CCM imesema Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa  Itikadi, Uenezi na Mafunzo ya chama hicho, CPA Amosi Makalla ametangaza hayo leo Mei 17 wakati akiuzungumza na  waandishi wa habari katika ofisi za CCM Lumumba, Dar es Salaam.

CPA Makalla amezitaja agenda za mkutano mkuu huo kuwa ni kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya kipindi cha miaka mitano 2020- 2025 ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali Mapinduzi ya Zanzibar, kupokea na kuzindua rasmi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025- 2030 na kufanya marekebisho katika Katiba ya CCM.

 

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Looking for a flexible way to earn extra income? This part-time opportunity allows you to work from home and make $570-$2400 each week. Perfect for anyone wanting to start something new—get your first payment by the end of the week. Tap into Finance, Economy, or Investing to begin!

    Get started here____>> https://Www.earnapp1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button