CCM yatoa kauli kifo cha kada Chadema

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimetoa pole kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kutokana na msiba wa mjumbe wa sekretarieti ya chama hicho, Ally Kibao na kuliomba jeshi la polisi kuhakikisha wahusika wanatiwa nguvuni.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla  ametoa salamu hizo za pole alipokuwa akizungumza katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Mirerani, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya siku sita Arusha na Manyara.

Isome pia:Serikali yatoa tamko matukio utekaji

Makalla ameliomba  jeshi la polisi kutimiza wajibu wake kwa kuhakikisha haki inapatikana katika hilo na kuhakikisha wahusika wanakamatwa.

“Nimeona katika vyombo vya habari kuanzia asubuhi mpaka sasa nitoe pole kwa chama cha CHADEMA kwa kumpoteza mmoja wa wajumbe wa sekretarieti Ally Kibao nimekuwa nikifuatilia, sisi ni vyama vya siasa linapokuja suala la ubinadamu siasa tunaweka pembeni,”amesema Makalla.

Habari Zifananazo

Back to top button