“Changamoto zisizuie biashara mtandao”

TAASISI ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) imesema licha ya kuwepo kwa fursa mbalimbali za biashara katika Soko Huru la Afrika (AfCFTA) bado zipo changamoto zinazotakiwa kufanyiwa kazi Ili zisizuie biashara kwa njia ya mtandao.

Mkurugenzi wa Bodi ya TPSF, Mercy Silla amesema hayo Dar es Salaam alipofungua mafunzo kwa wanawake na vijana namna wanavyoweza kutangaza biashara zao kwa njia ya kidigitali kupitia soko hilo na kufanya biashara kimataifa.

Mafunzo hayo ya siku mbili ya aratibiwa na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) Kwa udhamini wa SHIRIKA la Misaada la Kijerumani ( GIZ).

Akizungumza Silla amezitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na sarafu tofauti ya kila nchi, kila nchi kuwa na taratibu zake lakini pia kuwepo kwa taarifa mbalimbali za bidhaa kutopokelewa ipasavyo.

SOMA: TPSF yasisitiza matumizi ya teknolojia, ubunifu …

Amesema changamoto nyingine ni kuwa na kiwango kidogo cha uelewa kuhusu soko hilo, gharama za bidhaa kukinzana hususani katika biashara ya kidigitali na pia suala zima la hofu kwa matumizi ya teknolojia ya digitali kuhusu suala zima la usalama.

Amesema kuna haja ya mifumo kusomana na makundi hayo ya vijana na wanawake kuhakikisha wanajifunza Kwa kinachoendelea Ili Kutumia fursa za soko hilo.

Kwa upande wake Meneja wa Sera wa Biashara na Huduma kutoka EABC Geoffrey Kamanzi, akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa EABC, amesema Mpango wa Biashara wa AfCFTA tayari umeanza kufanya kazi na kuitaka sekta binafsi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuendelea kufahamisha jinsi ya kufanya biashara chini ya utaratibu wa AfCFTA.

SOMA: TPSF yaanzisha dawati la mazingira

Amesema EABC itaanzisha warsha kama hizo katika nchi nyingine za EAC ili kuimarisha namna ya kutumia mfumo wa kidijitali na kuimarisha utayari wa wafanyabiashara wadogo na WA kati (SMEs )kufanya biashara chini ya AfCFTA.

Amesema changamoto kama vile mifumo duni ya udhibiti, sarafu tofauti za kitaifa, huduma duni za wasafiri, uelewa mdogo, mkinzano wa gharama, masuala ya usalama na hofu ya ICT huzuia biashara kupitia biashara ya mtandaoni.

 

Habari Zifananazo

Back to top button