KIUNGO wa Simba, Ladack Chasambi amewaomba radhi viongozi, wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kwa kujifunga goli na kusababisha timu kukosa alama tatu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Fountain Gate.
Katika maelezo yake kupitia ukurasa wake wa mitandano ya kijamii, Chasambi amesema anwaomba radhi kwa uongozi wa klabu, benchi la ufundi, wachezaji wenzake na zaidi ya yote, mashabiki na wapenzi wa Simba kutokana na makosa aliyofanya kugharimu timu hiyo.
“Najua jinsi mnavyoipenda na kuiunga mkono klabu hii kwa moyo wote, ninaelewa matokeo yoyote yanayoiumiza timu, huwaumiza ninyi kama familia yetu.
“Sikutamani kabisa kufanya kosa hilo, lakini ni sehemu ya mchezo najifunza kutokana na hali hii kuwa mchezaji bora zaidi kwa ajili yenu na timu,” amesema.
Chasambi amesema anaahidi kujituma zaidi, kujifunza kutokana na makosa na kurejea akiwa na ari mpya ya kupigania mafanikio ya klabu ya Simba.
“Naahidi kujituma zaidi, naomba radhi kwa yeyote aliyeumizwa na kitendo changu, naomba muendelee kuniamini na kuniunga mkono,”amesema.
Kweli unaonyesha kujutia lakini nia yako haikua kujifunga ilikuwa kumrudishia mlinda mlango ili kuzua adui kupata lakini ikawa bahati mbaya !!!!!!!!!