CWT wahamasisha kujiandikisha uchaguzi mitaa

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) kimehamasisha wananchi kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa ikiwa ni pamoja na kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa.

Akizungumza katika bonanza la uhamasishaji uchaguzi hususan uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Makamu wa Rais wa Chama cha Walimu Tanzania, Suleiman Ikomba amewaomba watumishi wote hasa walimu na wananchi wote kujitokeza kujiandikisha.

SOMA: Tanroads kujiandikisha uchaguzi mitaa

“Kwa niaba yangu na Chama cha Walimu Tanzania, tunasema mama aendelee na tuko tayari kumuunga mkono. Kwanza, niwaombe walimu tuwe na jicho la pekee katika kuyasimamia mambo yanayoleta maslahi mbalimbali kwa taifa letu mojawapo likiwa ni kuhamasisha kujiandikisha kwenye daftari la mkazi,” amesema Ikomba.

Zoezi la kujiandikisha lilianza Oktoba 11 na linatarajiwa kutamatika Oktoba 20.

SOMA: Aweso ahimiza uchaguzi serikali za mitaa

Habari Zifananazo

Back to top button