WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk Pindi Chana amekutana na kufanya mazungumzo na machifu kutoka misitu ya Miteremko ya Safu za Milima ya Lyamba Lyamfipa kujadiliana namna ya uhifadhi endelevu wa eneo hilo la misitu.
Kikao hicho kimefanyika leo Oktoba 2,2024 Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa ambapo pamoja na mambo mengine amewapongeza machifu hao kwa juhudi zao za kuhifadhi eneo hilo muhimu kwa taifa katika utunzaji wa mazingira.
SOMA: Dk Chana akagua chanzo cha maji Miti Mbizi
Hifadhi ya Misitu ya Miteremko ya Safu za Milima ya Lyamba Lyamfipa ina vyanzo vingi vya maji ambayo yanatumiwa na wananchi kwa matumizi ya nyumbani na kwenye kilimo cha umwagiliaji na pia ndio chanzo cha mvua kwa eneo la Sumbawanga.